Wanafunzi_Shule ya Msingi_BukhaywaWanafunzi_Shule ya Msingi_Bukhaywa

Kiongozi Wa Muungano Wa Walimu Wa Shule Za Upili KESSHA Kaunti Ya Kakamega Ambaye Pia Ni Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Upili Ya Bukhaywa Michael Amukoha Amepongeza Hatua Ya Serikali Kufungua Shule Muhula Wa Pili Baada Ya Likizo Ndefu Iliyotokana Na  Janga La Covid19 Tangu Mwezi Machi Mwaka Jana

Akizungumza Afisini Mwake Na Kituo Hiki Amukoha Amesema Licha Ya Shule Kufunguliwa Kuna Changamoto Ambazo Bado Zinakumba Shule Mbalimbali Ikiwemo Shule Yake Ya Upili Ya Bukhaywa

Amukoha Ametaja Swala La Mita Moja Na Uhaba Wa Madarasa Ya Kutosha Kama Tatizo Kubwa Kwa Sasa

Amesema Licha Ya Wanafunzi Kurejea Bado Hawajarejesha Mafikirio Ya Shule Kwani Wengi Wao Wamekuwa Wakifanya Shughuli Kando Na Kalenda Ya Masomo

Amesema Wanafunzi Walio  Na Ujauzito Wataruhusiwa Kwendelea Na Masomo Yao Kwani Si Makosa Yao

Ametaka Serikali Kuleta Pesa Kwa Haraka Kwa Shule Ili Kusaidia Kuafikia Vigezo Vya Wizara Ya Afya Ambavyo Vinahitaji Senti Za Kutosha

Hata Hivyo Kuhusiana Na Idadi Ya Wanafunzi Walio Na Ujauzito Katika Shule Hiyo Amukoha Amesema Kwa Sasa Bado Hawajapata Idadi Kamili Kwani Ndio Wanafunzi Wanarejea Shuleni

 Ila  Amesema Kutokana Na Takwimu Za Kwanza Ni Wanafunzi 6 Kati Ya Watahiniwa 162 Walio Na Ujauzito Katika Shule Hiyo Ya Upili Ya Bukhaywa

Kwa Upande Wake Naibu Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Ya Bukhaywa Seth Litiema Amesema Licha Ya Shule Kufunguliwa Shule Hiyo Inapitia Changamoto Si Haba Ikiwemo Ukosefu Wa Madarasa Ya Kutosha Kwa Sasa Baadhi Ya  Wanafunzi Wakilazimika Kuketi Chini Ya Kivuli Kwani Bado Madarasa Yanayojengwa Na Hazina Ya Maendeleo Kwenye Eneo Bunge La Shinyalu Cdf Bado Madarasa Hayo Hayajakamilika

Litiema Amesema Ni Kisa Kimoja Cha Mimba Ambacho Kimeeipotiwa Shuleni Humo Ila Tayari Hatua Zimechukuliwa Ili Kulinda Mwanafunzi Huyo Aendeleze Masomo Yake

Samuel Malova Ni Mojawapo Ya Wazazi Tuliozungumza Nao Na Kutoa Maoni Yake Kwa Matayarisho Ya Shule Ya Mwanawe Shule Ya Upili Ya Bukhaywa

Samuel Amesema Ametosheka Na Maandalizi Ya Shule Hiyo Huku Akiitaka Serikali Kuharakisha Ujenzi Wa Madarasa Zaidi Ili Kukimu Kigezo Cha Mita Moja Kwa Wanafunzi.

Na Ripota Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE