BEKI Mkenya Abud Omar Khamis anaendelea kufanyia Ionikos Nikeas kazi safi kwenye Ligi ya Daraja ya Pili nchini Ugiriki baada ya kufunga bao la pekee timu hiyo ikizamisha Panachaiki 1-0 Jumapili.

Ionikos, ambayo iliingia mchuano huo ikiuguza vichapo mikononi mwa Panachaiki katika mechi mbili zilizopita, iliendeleza rekodi yake nzuri ya ugenini dhidi ya wapinzani wao hadi mechi nne katika tano walizokutana tangu mwaka 1999.

Omar,28, alipachika bao hilo dakika ya tisa ya majeruhi.

Na kule ugaibuni MANCHESTER City walipiga hatua kubwa katika kuweka wazi maazimio yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu baada ya kupokeza mabingwa watetezi Liverpool kichapo cha 4-1 mnamo Jumapili usiku.

Mchuano huo ulishuhudia chipukizi Phil Foden akitamba zaidi uwanjani huku masihara ya kipa Alisson Becker yakichangia pakubwa masaibu ya Liverpool wanaotiwa makali na kocha Jurgen Klopp.

Hayo yakijiri KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba fowadi na nahodha Harry Kane sasa ataweza kuvunja kila rekodi kwenye soka ya Uingereza baada ya Mwingereza huyo kupona haraka na kurejea uwanjani.

Marejeo ya nyota huyo yalichochea waajiri wake kucharaza West Bromwich Albion 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Februari 7, 2021.

 Story by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE