TAARIFA ZA SPOTI IJUMAA 04/01/2019

AARIFA ZA MICHEZO IJUMAA 4/01/2019

KITAIFA

SHIRIKISHO LA RIADHA NCHINI ATHLETIC KENYA ALMAARUFU A.K LIMEPIGA MARUFUKU MBIO ZINAZO-ENDELEZWA NA WADAU TOFAUTI BILA KUPATA RUHUSA KUTOKA AFISI KUU YA RIADHA NCHINI.KWENYE TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI A.K IMESEMA KUWA ATAKAYEPATIKANA AKIENDESHA SHUGHULI ZOZOTE ZA RIADHA BILA IDHINI ATATIWA MBARONI NA KUFUNGULIWA MASHTAKA.
NA HIVYO A.K IMEWATAKA WADAU HUSIKA KUPATA IDHINI YA SHIRIKISHO HILO KABLA YA KUANDAA HAFLA ZOZOTE ZA RIADHA ILI KULINDA MASLAHI YA WANARIADHA NCHINI.

KLABU ILIYOPANDISHWA NGAZI KATIKA LIGI KUU YA KENYA MSIMU HUU KENYA COMMERCIAL BANK K.C.B IMEWASIMAMISHA KAZI NAIBU WAKUFUNZI WA KLABU HIYO ELVIS AYANY NA EZEKIEL AKWANA BAADA YA WAWILI HAO KUSHINDWA KUMSAIDIA KOCHA FRANK OUNA KUSAJILI USHINDI WOWOTE BAADA YA KUCHUKUA MIKOBA YA KLABU HIYO HUKU WAKIFANIKIWA KUPATA ALAMA MOJA TANGU KOCHA OUNA NA NAIBU HAO KWANZA KUINOA KLABU HIYO.
K.C.B ITAWAKARIBISHA KARIOBANGI SHARKS HIYO KESHO KATIKA MECHI YA LIGI KUU KENYA.

KLABU YA AFC LEOPARDS IMEPIGWA JEKI BAADA YA MSHAMBULIZI BONVENTURE KAHEZA KURUHUSIWA KUCHEZA KATIKA LIGI KUU YA KENYA.
KAHEZA AMBAYE ALIHAMIA INGWE DESEMBA MWAKA JANA 2018 HAKUWA NA LESENI YA KUSHIRIKI LIGI KUU KENYA NA HIVYO HAKURUHUSIWA KUCHEZA LAKINI KWA SASA KENYA PREMIERE LEAGUE IMEMPA LESENI YA KUSHIRIKI.KAHEZA ALIHAMIA INGWE KUTOKA KWA MIAMBA WA SOKA TANZANIA SIMBA FC.

MKUFUNZI WA KLABU YA WANAMVINYO TUSKER ROBERT MATANO AMEELEZEA NIA YA WANAVILEO HAO KUSHINDA TAJI LA LIGI KUU KENYA MSIMU HUU BAADA YA MSURURU WA MATOKEO MAZURI.
MATANO AMESEMA KUWA TUSKER IPO TAYARI KUKABILIANA NA YEYOTE KATIKA LIGI KUU KENYA.
KWA HIVI SASA TUSKER WAPO KATIKA NAFASI YA TATU KWA ALAMA KUMI ZIKIWA ALAMA TATU NYUMA YA VIONGOZI WA LIGI MATHARE UNITED.

KIMATAIFA

MATUMAINI YA KLABU YA LIVERPOOL KUFUNGUA MWANYA WA ALAMA NYINGI KATIKA LIGI KUU UINGEREZA NA MATUMAINI YA KUSHINDA LIGI YA UINGEREZA ILIKATIZWA HIYO JANA USIKU BAADA YA BINGWA MTETEZI MANCHESTER CITY KUWASHINDA LIVERPOOL MAGOLI 2-1 UGANI EL ETTIHAD.
SERGIO AGUERO ALIIFUNGIA CITY BAO LA KWANZA KIPINDI CHA KWANZA KABLA YA ROBERTO FIRMINO KUSAWAZISHA NAYE LEROY SANE AKAZAMISHA MELI YA LIVERPOOL YA KUTOSHINDWA KATIKA LIGI KUU UINGEREZA KWA KUIFUNGIA CITY BAO LA PILI.SASA LIVERPOOL INAONGOZA LIGI KWA ALAMA 54 ALAMA 4 JUU YA MANCHESTER CITY WALIO NA ALAMA 50.

MATUMAINI YA REAL MADRID KUPUNGUZA ALAMA DHIDI YA FC BARCELONA KWENYE LIGI KUU UHISPANIA YALIDIDIMIA JANA BAADA YA KUTOKA SARE YA 2-2 DHIDI YA VILLARREAL HIYO JANA USIKU.
ALIYEKUWA NYOTA WA ARSENAL SANTI CAZORLA ALIIFUNGIA VILLARREAL MAGOLI YOTE MAWILI HUKU KARIM BENZEMA NA RAFAEL VERANE WAKIIFUNGIA REAL MADRID.

NYOTA WA KLABU YA CHELSEA NGOLO KANTE NA NAHODHA WA KLABU YA CHELSEA CESAR AZIPILICUETA WAMEMKARIBISHA KIKOSINI SAJILI MPYA KUTOKA BORUSSIA DORTMUND CHRISTIAN PULISIC.
CHELSEA IMEMSAJILI PULISIC KWA KIMA CHA MILIONI 58 NA BADO ATASALIA DORTMUND HADI MSIMU UKAMILIKE KABLA YA KUJIUNGA NA WANA BLUES.
PULISIC MWENYE UMRI WA MIAKA 20 RAIA WA MAREKANI AMEKUWA NA MSIMU MZURI DORTMUND NA HIVYO ATASALIA KULE HADI MWISHONI MWA MSIMU.

BY SAJIDA JAVAN …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *