Tuko katika hawamu ya mwisho ya kufanyia majaribio dawa ya kutibu korona

Ni usemi wa mwenyekiti wa madaktari wa kienyeji kaunti ya Bungoma Sindani Barasa,

Kwenye usemi na taarifa kwa wanahabari nje ya ofisi yake katikati ya mji wa Bungoma kaunti ya Bungoma, Sindani amedai kuwa ipo haja ya serikali kuwahusisha moja kwa moja madaktari wa tiba za kiasili katika tafiti za pamoja ili kupata suluhu la jinamizi la korona

Daktari huyo wa kienyeji aidha amewataka wananchi kuikumbatia dawa hiyo pindi tu itakapouidhinishwa na kufikishwa sokoni

Sindani aidha amefichua kuwa tangia kutangazwa kwa janga hatari la korona yeye pamoja na madaktari wenzake wa kienyeji kutoka Kenya na Uganda wamekua wakifanya sampuli mbalimbali za madawa  ili kupata suluhu kwa kero la korona

Hadi kufikia sasa daktari sindani amesema kuwa yeye binafsi amekua akitumia dosia hiyo ili kujikinga na maambukizi ya korona na ameona mafanikio makubwa.

Tangia machi mwaka jana janga hatari la korona limezidi kuwa kero kote duniani huku taasisi mbalimbali za kitaalam na mambo ya afya na madawa kote duniani zikizidi kufanyia majaribio dawa mbali mbali ili kuhakikisha kuwa dawa kamili ya kudhibiti janga lenyewe inapatikana.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE