Waziri wa elimu Profesa George Magoha, ameipongeza shule ya msingi ya Bungoma DEB kuwa iliyo miongoni mwa shule ambazo zinazingatia kikamilifu masharti ya wizara ya afya kuzuia maambukizi ya Korona nchini.

Akizungumza alipozuru shule hiyo, waziri Magoha amesema japo kuwa shule hiyo ni ya pili kwa ukubwa wa idadi ya wanafunzi nchini, imeafikia masharti ya wizara ya afya ikiwemo sehemu za kunawia mikono, maski ka kila mwanafunzi na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani ili kuepusha msambao wa virusi vya korona.

Wakati uo huo Magoha amerejelea msimamo wa wizara ya elimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaodaiwa karo hawarudishwi nyumbani.

 Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE