Lubao FM | 102.2 Hz

Month: February 2021

Wezi kula nyasi Westkenya eneobunge la Malava Kaunti ya Kakamega

Wenyeji wa kijiji cha Westkenya eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wamejionea kioja baada ya watu wawili ambao ni wahudumu wa baa moja eneo hilo kugeuka kuwa wazimu kufuatia madai ya kushiriki wizi eneo hilo. Wawili hao ambao ni mwanamme mwenye umri wa miaka 36 na mwenzake wa kike wa miaka 27 wakiwa wafanyikazi …

Wezi kula nyasi Westkenya eneobunge la Malava Kaunti ya Kakamega Read More »

Wanafunzi kupokezwa baiskeli katika shule ya upili ya Mtakatifu Monica Lubao

 Ni afueni kubwa kwa wanafunzi wa shule ya upili ya Mtakatifu Monica Lubao baada ya wanafunzi 100 kufaidika na mradi wa Baiskeli aina ya Bufallo kutoka kwa shirika la kibafsi la World Bicycle relief ambalo limewapokeza baiskeli hizo ikiwa ni mara ya pili baada ya kupokezwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 Akizungumza na kituo …

Wanafunzi kupokezwa baiskeli katika shule ya upili ya Mtakatifu Monica Lubao Read More »

Mauti Eneo bunge la Matungu Baada ya Mwanafunzi wa Darasa la Nane Kujitia Kitanzi

Biwi  la  simanzi     lingali  limeigubika  familia  moja  kutoka  kijiji  cha  Mungakha wadi  ya  Namamali   eneobunge  la  Matungu  kaunti  ya  Kakamega   baada  ya  mwanafunzi  wa  darasa  la  nane  katika  shule  ya  msingi  ya  Mungakha  kujitia  kitanzi  mapema  leo  asubuhi  na  kuaga  dunia….  Kulingana  na  wazazi  wa  mtoto  huyo  ni  kwamba  mwanao  mwenye  umri  wa  miaka  kumi  …

Mauti Eneo bunge la Matungu Baada ya Mwanafunzi wa Darasa la Nane Kujitia Kitanzi Read More »

Wanasaikolojia Kuajiriwa katika shule ili Kuwasaidia wanafunzi walio na msongo wa mawazo

Walimu pamoja na washikadau wote katika sekta ya elimu wameshauriwa kuwa karibu na wanafunzi na kuwapa nafasi ya kujieleza ili kuepusha visa vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea kushuhudiwa nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mamlaka ya kudhibiti ubora wa elimu nchini (Kenya National Qualifications Authority) Dakt Juma Mukhwana, visa vingi vya utovu wa nidhamu vinavyoshuhudiwa …

Wanasaikolojia Kuajiriwa katika shule ili Kuwasaidia wanafunzi walio na msongo wa mawazo Read More »

Kina Mama Kaunti ya Bungoma kupata Pesa na Kushauriwa kujiandikisha na kikundi cha hazina yao ya Women Enterprise Fund

Akina mama Kaunti ya Bungoma wameshauriwa kujisajili katika vikundi na kupewa pesa za mikopo kutoka hazina ya akina mama ya Women Enterprise Fund ili kujiendeleza kiuchumi. Akizungumza wakati wa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita nukta sita kwa vikundi vya akina mama, Charles Mwirigi ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Hazina hiyo, amesema idadi ya …

Kina Mama Kaunti ya Bungoma kupata Pesa na Kushauriwa kujiandikisha na kikundi cha hazina yao ya Women Enterprise Fund Read More »

Wafanyikazi Wa Chuo Kikuu cha moi kushiriki Mgomo

Wafanyakazi wa Chuo cha Moi wakiwemo wahadhiri na, wametishia kuandamana kwa kile wanasema kilio chao hakisikizwi na usimamizi wa Chuo hicho. Wakiongea nje ya afisi kuu ya Chuo hicho zilizoko behewa la Kesses, wafanyakazi hao wamelalamikia masuala kadhaa ikiwemo ukosefu wa Bima ya Afya, kucheleweshwa kwa mishahara na marupurupu yao. Kwa upande wake Naibu chansela …

Wafanyikazi Wa Chuo Kikuu cha moi kushiriki Mgomo Read More »

Wavuvi wa Ziwa Victoria Kaunti ya Busia kutoa Malalamishi kwa vikosi vya Coast Guard na Kenya Maritime Authority

Wavuvi katika ziwa Victoria Kaunti ya BUSIA wamevisuta vikali vikosi vya Coast Guard na Kenya Maritime Authority kwa madai ya kuwanyanyasa. Wakiongozwa na Mwenyekiti Wa fuo za ziwa Victoria Sylvester Kaywa, wamevitaka vikosi hiyo kusitisha mara moja zoezi LA kuwatia mbaroni wavuvi kwa makosa madogo madogo na badala yake watafute kuwepo mazungumzo kumaliza utata unaowakumba …

Wavuvi wa Ziwa Victoria Kaunti ya Busia kutoa Malalamishi kwa vikosi vya Coast Guard na Kenya Maritime Authority Read More »

Wazazi Kulalama Kwaniaba ya Wana wao shuleni kaunti ya Bungoma

Baadhi ya wazazi katika shule ya upili ya Wasichana ya Cardinal Otunga kwenye Kaunti ya Bungoma wameushtumu uongozi wa shule hiyo kwa kuwatimua wanafunzi watano wa kidato cha tatu kwa madai ya kutumia dawa za kulevya. Baadhi yao waliozungumza na Kituo hiki kwa njia ya simu, wameikosoa Bodi ya shule hiyo kwa kuwalazimisha wanafunzi kukubali …

Wazazi Kulalama Kwaniaba ya Wana wao shuleni kaunti ya Bungoma Read More »

Jamii Ya Mulembe Yatakiwa Kuungana Kutoa Rais Mwaka 2022

Viongozi wa jamii ya mulembe wametakiwa kuungana na kutoa kiongozi mmoja atakaye peperusha pendera ya Urais ifikapo mwaka 2022 ili aungwe mkono na jamii yote kwa ujumla . Wakizungumza na idhaa hii mjini Malava wanabodaboda wakiongozwa na Isaac Mukaramoja wamehoji kuwa jamii zote nchini zimeungana na zimekuwa zikiombea mgombea wao kila mwaka huku jamii ya …

Jamii Ya Mulembe Yatakiwa Kuungana Kutoa Rais Mwaka 2022 Read More »

Siasa Matungu Kaunti ya Kakamega

Seneta mteule kutoka kaunti ya Kakamega Naomi Shiyonga amewarai wakazi wa Matungu kujitokeza kwa wingi tarehe 4 mwezi ujao  kushiriki  uchaguzi mdogo utakaofanyika ili kumchagua mbunge wao baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Justus Murunga kufariki. Akizungumza baada ya kuvitembelea vikundi vya akina mama kwenye  wadi ya Namberekeya Shiyonga amewataka wakazi hao kujitokeza kwa …

Siasa Matungu Kaunti ya Kakamega Read More »

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE