Amani na umoja ndio kauli mbiu uliotawala mazishi ya mama ashura saisi mkewe naibu gavana wa kaunti ya vihiga kwenye ibaada iliyoandaliwa katika soko la Cheptulj eneo bunge la Hamisi 

Katika ibaada iliyohudhuriwa na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, gavana wa Vihiga Wilber Ottichilo na gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya miongoni mwa viongozi wengineo 

Viongozi mbalimbali toka Vihiga kutoka kwa waakilishi wadi hadi wabunge walimsihi kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwaunganisha gavana wa Vihiga na naibu wake ambao wamekuwa na taofauti za uongozi na kulemaza ajenda ya maendeleo kaunti hiyo

Ni wito ambao gavana Ottichilo alikubali kwa kauli moja na kutoa msamaha kwa naibu wake na kumtaka kushirikiana naye kwendeleza ajenda ya maendeleo

Kwa upande wake naibu gavana amemuomboleza mkewe kwa kummininia sifa kama mama aliyetosha kwa upendo wa familia

Katika wito wa kuwaleta pamoja ulienezwa na gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya akiwataka viongozi wa kaunti ya Vihiga kuzika tofauti zao za kisiasa na kuwafanyia wanainchi maendeleo

Hata hivyo Oparanya amepuzilia mbali mwito wa viongozi wa Mulembe kuja pamoja pasina kuhusisha jamii nyinginezo ili kutwaa uongozi wa taifa hili kwenye uchaguzi mkuu ujao akisema hilo halitawezekana

Hata hivyo amewataka viongozi kutohusisha siasa katika ziara ya rais Uhuru Kenyatta katika mkoa wa Magharibi mwa Kenya ambayo inaweza kuchochea rais kususia ziara hiyo na kuwadhuru wakaazi wa magharibi mwa Kenya kiujumla

Hata hivyo tofauti za uongozi baina ya gavana Ottichilo na naibu wake daktari Patrick Saisi zimezikwa kwenye kaburi la sahau sahaulika baada ya kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwaleta pamoja na kusalamiana jambo ambalo limeshabikiwa na wakaazi wa kaunti hiyo.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE