Wakaazi wa lubao wanashauriwa na viongozi wao wa usalama kuhakikisha kwamba hawabaki nyuma kuwaelimisha watoto wao kwa kuwapeleka shuleni.

Wakizungumza katika ibaada ya mazishi ya mwenda zake aliyekuwa fundi shupavu mzee joel tieni imonje katika kijiji cha lubao jumanne hii 12-01-2021,  wazee wa mtaa wa wagukha na imuliru  bw. Kutwa shivisi na bw. Sisko sayi walikashifu kitendo cha wazazi kuwalegeza wanao wanapokosa nidhamu kwa kuwatetea.

Naibu chifu wa mtaa wa lubao suluveyi ashiono kwa upande wake anatoa tahadhari kwa mwanafunzi ambaye bado hajarejea shuleni kufanya hivyo hata kama ni mja mzito na kukashifu kitendo cha watoto kuenda kutenya kuni msituni na kujiweka katika hatari ya kunajisiwa na watu wenye nia mbaya.

Akiongezea naibu chifu huyo anawaonya vikali wanaume na wanawake wenye tabia mbaya ya kutojilinda na kujiheshimu badalake wanaanza kuwinda mijuzi za inje.

Story by Wycliffe Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE