Wakulima wa kahawa kutoka  eneo la magharibi mwa Kenya wamehofia kuwa huenda wakakosa kupokea mgao wa fedha wa shilingi bilioni tatu zilizotolewa na serikali ya taifa ili kusaidia kuboresha kilimo hicho.

Afisa mkuu mtendaji wa chama cha ushirika cha Kimama eneobunge la Mlima Elgon Ben Mulupi anasema vyama vingi vya ushirika eneo hili, huuza zao la kahawa  kwenye kampuni za kibinafsi hatua anayosema huenda ikawanyima nafasi kupata fedha hizo.

Aidha Mulupi amewataka wakulima kuwekeza fedha za kahawa kwa elimu ya wanao kando na kuhakikisha wanafwata ratiba ya kilimo hicho ili kuboresha zao hilo.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE