Viongozi wa makanisa ya kiroho katika kaunti ya Busia wameitaka serikali kupitia kwa wizara ya afya kulegeza sheria ya kutotangamana ili kuwaruhusu kuendeleza shughuli za maombi kwa wahumini wao jinsi inavyofanyika kila wakati ikiwemo kuwawekea mikono wanapokemea mapepo.

Viongozi hao wamesema kuwa kama desturi katika makanisa ya kiroho wanakemea mapepo na kuwawekea mikono wahumini wao na sasa wanakabiliwa na wakati mgumu wakati wa kuendeleza hafla za maombi.

Wakiongea na waandishi wa habari katika kijiji cha Bukadanyi Nambale chini ya uongozi mwanzilishi wa kanisa la Free Pentecostal kanda ya Afrika Mashariki askofu Timothy Kokonya wamesema kuwa idadi kubwa ya wenyeji hukabiliwa na matatizo yanayotokana na ushirikishina hali ambayo inapaswa kutatuliwa kwa maombi na sasa imekuwa vigumu kuwashughulikia.

Aidha wamesisitiza kuwa kanisa linafanya jukumu kubwa la kuombea taifa na serikali hivyo basi sio vyema kuwekewa vikwazo.

Kwa sasa hao wamefichua kuwa tangu kuzuka kwa janga corona asili mia kubwa ya wahumini wamepungukiwa na imani na hatawengine wao kujiingiza kwa kwenye mienendo potovu hali ambayo huenda ikaongeza utovu wa usalama.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mmoja wa manabii wa kanisa hilo Wycliffe Wafula almaarufu Ochomotir ambaye amekuwa akiendesha shughuli ya kukabiliana na matatizo ya ushirikina katika jamii.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE