Washkadahu kwenye sekta ya miwa nhini wanazisuta kampuni za kibinafsi kwa kushirikiana na matapeli kuwanyanyasa wakulima
Wakiongozwa na Mwanaharakati wa maendeleo eneobunge la Navakholo Dan Mustotso Mmayi vyongozi hao wanadai kuwa hili limefanya wakulima kupoteza Imani na kampuni hizo
Mwanachama huyo kwenye kamati ya shirika linaloangazia ufufuzi wa sekta ya miwa eneo hili Kakamega sugarcane Growers Cooperative amesema kuwa kama vyongozi watafanya wawezalo kukomesha dhulma hizo na kurejesha hadhi ya miwa kwa mkulima
Mmayi amekanusha kuwa ukosefu wa malihgafi(raw materials) ndicho chanzo cha kuanguka kwa baadhi ya viwanda vya sukari nchini
Kiongozi huyo hata hivyo amepongeza hatua ya rais kufungua baadhi ya maeneo nchini yalokuwa yamefungwa kwenye vita dhidi ya msambao wa virusi vya Corona
By James Nadwa