Mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake eneo bunge la Lurambi  bi Agnes Barasa amewahimiza wenyeji haswa akina mama kujiunga kwenye makundi na kutumia mvua inayonyesha kwa sasa  kupanda vyakula vinavyochukua muda mfupi kama njia moja ya kukuza uchumi wa sehemu hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja  akina mama wajane kule Lurambi kuwahamasisha njia za kutoka kwenye uchochole,bi Barasa ametaja kuweko kwa soko la kutosha kwa vyakula hivyo na kuwataka kutumia fursa hiyo kujikamua kutoka katika lindi la uchochole.

Wakati huo uo kiongozi huyo amewataka akina mama hao kupanda mboga za kienyeji kwa wingi za kuuza na kutumia akisema kuwa  ni tiba ya mwili .

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE