Ni afueni kwa wakaazi wa Lubao na viungani mwake baada ya Kuzinduliwa hiyo jana mradi wa Solar kusaidia nguvu za umeme kwa usambazaji wa maji kwenye sehemu mbalimbali

Katika hafla iliyoandaliwa ijumaa katika shule ya upili ya Lubao na kuhudhuriwa na mbunge wa Shinyalu Justus Kizito Mugali umegharimu shilingi milioni 1.7 kutoka kwa shirika la KIWASH na wadhamini wengineo jinsi anavyosema mwakilishi wa kiwash mhandisi mutie

Mwakilishi wadi ya Isukha kazkazini Hellemina Llanziva akiusifia mradi huo na kurai serikali ya kaunti ya Kakamega kupitia KIWASH kushirikiana naye ili kuona kuwa wakaazi wanapata tenki kubwa la maji hayo kusambazwa maeneo mbalimbali ikiwemo shule zilizoko karibu

Naye afisa mkuu mtendaji wa kituo hiki cha lubao fm frederick witaba akimsihi mwakilishi wadi ya Isukha Kazkazini kufwatilia makadirio ya bajeti ya kaunti ya Kakamega baada yake kuwasilisha wazo la usambazwaji wa maji viungani mwa swhemu zilizo karibu na kituo hiki ili kuafiki azimio la gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya la kusambaza maji “Matsi Khumukuru

Wakati uo huo mbunge wa Shinyalu amesifia mradi huo wa maji na kuitaka kamati andalizi kuchunga mradi huo kutoharibiwa

Kizito amesifia utendakazi wa kituo hiki cha Lubao Fm na kuwasihi waekezaji kujitokeza na kutoa hisani mbalimbali ili kwendeleza kazi bora inayofanywa na kituo hiki

Wakati uo huo kizito amewataka wakaazi wa Shinyalu kuwa na subira huku akiendeleza miradi ya ujenzi wa shule mbalimbali kwenye eneo bunge la Shinyalu

Hata hivyo amemrai jaji mkuu wa mahakama nchini Martha Koome kuwachunguza baadhi ya majaji ambao wanafanya kazi kama wanahatakati kwa kutofwata sheria 

Akikosoa uamuzi wa mahakama ya juu uliyofanywa na majaji 5 kwa kusimamisha mchakato wa kubadilisha katiba kupitia mfumo wa BBI huku akimtetea rais Uhuru Kenyatta asiyekuwa na hatia licha ya uamuzi huo kumlenga na kusema ana imani uamuzi huo utabadilishwa na mahaakama ya rufaa na kurejelea mchakato wa kubadilisha katiba 

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE