Makala ya 33 ya mashindano ya  kombe la kimataifa ya Africa AFCON yatakayoshindaniwa yataandaliwa nchini Cameroon kati ya Januari 9 na Februari 6 mwaka wa 2022.

Kutokana na mipango iliyowekwa ya  baraza kuu la CAF kupitia kwa njia ya mtandao droo ya kipute hicho itaandaliwa juni 25 , 2021 ambapo timu 24 zitapangwa kwa makundi 6 ya timu nne kila moja .

Mataifa 23 yamejikatia tiketi kwa mkaragazano huo  wa  mwakani ,huku nafasi moja iliyosalia ikijazwa na aidha Sierra Leone au Benin zitakazochuana  kati ya Mei 31 na Juni 5 mwaka huu ,ikizingatiwa kuwa  pambano hilo liliahirishwa wiki jana baada ya wageni Benin kutoa lawama kuhusu matokeo ya Covid 19 kwa wachezaji wake.

Nchi zilizopewa tiketi ya mashindano ya mwakani ni 23 wakiwemo  mabingwa watetezi Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Comoros, Egypt, , Ethiopia, Gabon, Equatorial Guinea Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, Senegal, Sudan, Tunisia na Zimbabwe .

By Austin Shambetsa 

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE