Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 22 amefariki papo hapo huku mhudumu wa Bodaboda aliyekuwa amembeba akivunjika mguu baada ya kugongwa kwa nyuma na Lori eneo la Aget kwenye barabara ya Busia-Malaba.
Kulingana na Babake mzee Benedict Emokor, mwanawe Belinda Amoit Emokor ambaye alikamilisha mtihani wake wa kidato cha nne 2019 katika shule ya upili ya st Joseph Chakol, alikumbana na mauti yake majira ya jioni alipokuwa akitoka kibarua mjini Busia.
Kilio cha familia hii imeungwa mkono na majirani ambao wameitaka idara ya usalama kusaidia kupata gari iliosababisha ajali hiyo.
Pia wameelekeza kidole cha lawama kwa mamlaka ya Barabara nchini KENHA kwa kushindwa kuweka matuta kwenye barabara hiyo ambayo imeangamiza maisha ya watu wengi kufikia sasa.