Akina mama wa chama cha ANC eneo bunge la Lurambi wamewataka viongozi kuzingatia jamii ya walemavu na kuona kwamba wanainuliwa kiuchumi
Wakiongozwa na mwenyekiti Ruth Ombayo walipomtembelea mama Violet Anangwe katika kijiji cha Emayungu ambaye anawakilisha walemavu katika wadi ya Butsotso ya kati wamesema ni njia moja ya kuhamasisha wananchi mashinani umhimu wa kumuunga mkono kinara wa ANC Musalia Mudavadi kukwamua uchumi wa kenya
Ni usemi ulioungwa mkono na mwenyekiti wa wadi ya Butsotso ya kati Lilian Nafula
Bi Ombayo vile vile amewataka viongozi kushirikiana kuendeleza elimu ya watoto kutoka jamii zenye changamoto za kifedha kama njia ya kuinua jamii
BY Linda Adhiambo