Aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge cha Matungu kwa tiketi ya ODM David Aoko Were amewasilisha kesi katika mahakama ya Kakamega  kupinga kuchaguliwa kwa mgombea wa ANC Peter Oscar Nabulindo kama mbunge wa eneo hilo akidai kuwa shughuli za uchaguzi zilikumbwa na udanganyifu.

Were kwa sasa anaitaka mahakama kubatilisha kuchaguliwa kwa Nabulindo

Katika stakabadhi zilizowasilishwa katika mahakama ya kakamega, Were amedai kuwepo na makosa wakati wa zoezi la kupiga na kuhesabu kura yaliyoathiri matokeo ya uchaguzi huo.

Katika kesi hii, Were ameishitaki tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC,  afisa aliyesimamia uchaguzi huo John Kiplagat na mbunge wa Matungu Peter Nabulindo.

Were anawakilishwa na  Marende and Nyaundi advocates katika kesi hii.

By  Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE