Chama cha Ford Kenya na kile cha ANC vitashirikiana kwenye chaguzi ndogo za Kabuchai kaunti ya Bungoma na Matungu kaunti ya Kakamega.

Akizungumza alipoandamana na mgombezi wa chama cha Ford Kenya kwenye uchaguzi mdogo wa Kabuchai Majimbo Kalasinga katika afisi za IEBC, Seneta wa Bungoma na Kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula amesema ushirikiano wa Ford Kenya na ANC ubalenga kuafiki umoja wa jamii ya mulembe mbele ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kwa upande wake kinara wa ANC Musalila Mudavadi aliyekuwa ameandamana na Wetangula, amewaomba viongozi wengine kuunga mkono mwelekeo wa FORD Kenya na ANC ili kuipa jamii hiyo usemi wa kisiasa.

Chama cha Ford Kenya kitawasiloshwa na Majimbo Kalasinga kutetea kiti cha ubunge wa Kabuchai kilochoachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo James Mukwe mwaka uliopita.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE