Baadhi ya wafwasi wa Chama Cha ANC wilayani Navakholo wameshtumu Chama Cha ODM kwa kutumia mbinu ghushi kwenye kampeni za kushinda uchaguzi mdogo wa Matungu
Wakiongozwa na Ben Shibona wafwasi hao wamemtahadharisha naibu mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni gavana wa Kakamega dhidi ya kulazimisha wakaazi wa Matungu kumchagua mgombea wao ambaye ni David Were
Shibona vile vile ametilia shaka agizo la waziri wa elimu la kuwapiga marufuku wanaabari dhidi ya kuzuru shule wakati huu
Aidha ameonyesha kutoridhika na mikakati iliyowekwa na serikali kuzuiya kusambaa kwa virusi vya Corona haswa kwenye shule za humu nchini
Story by James Nadwa