Huku wakenya wakiadhamisha sherehe za Madaraka ya 58 tangu wapate madaraka tarehe moja juni, wenyeji wa kaunti ya Kakamega wamelalamikia kutelekezwa na serikali kuu kwa upande wa miradi za maendeleo.

Wakiongozwa na Boaz Shikuku Mukami  wanasema kuwa miradi za serikali kuu zimeegemea upande mmoja  huku eneo la magharibi ikiwemo kaunti ya Kakamega ikitelekezwa kimaendeleo.

Kulingana na wenyeji hao wanasema kuwa hakuna mradi wowote kutoka kwa serikali kuu umepelekwa  kaunti hiyo huku ujenzi wa barabara ya Lurambi kupitia nambacha hadi musikoma ukikwama .

Wenyeji hao pia wamelalamikia kufungwa kwa kiwanda cha sukari cha Mumias huku rais akizindua miradi mipya eneo la nyanza.

Ni kauli iliyotiliwa mkazo na viongozi wa kisiasa eneo hilo akiwemo mbunge wa Lurambi askofu Titus Khamala na mwenzake wa Ikolomani Benard Shinali.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE