Ipo haja kwa serikali ya kaunti ya Kakamega kupitia viongozi wa wadi kusaidia kutengeneza barabara na vivukio eneo hilo ili kuwezesha usafiri.

Katika kijiji cha Mutseywe wananchi iliwabidi kujitokeza na kutengeneza kivukio kwenye barabara ya kutoka Emurumba kuelekea Ejinja eneo bunge la Lurambi huku wakilaumu mwakilishi wadi wa Butsotso ya kati kwa kuzembea.

Wakiongozwa na Jacob Otinga wakaazi hao wamesema kuwa wamechukua hatua hiyo mbele ya ufunguzi wa shule kwani kuvukio hicho kinaunganisha watoto kutoka sehemu za Ejinja na Murumba wasisumbukane.

Sasa wananchi hao wanaitaka serikali ya Kakamega kuilima barabara hiyo na kuweka daraja la kudumu kwa sababu inasaidia si tu wanafunzi hata wagonjwa na wamama wajawazito kuenda katika zahanati ya Shiyunzu.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE