Barcelona wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, lakini uhamisho wa bure wa kiungo huyo aliye na umri wa miaka 32- utategemea ikiwa klabu hiyo ya Nou Camp itafanikiwa kumshawishi mshambuliaji mwenzake wa Argetina Lionel Messi, 33, kusalia nao. 

Na Kule Old Trafford Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer huenda akawauza wachezaji Jesse Lingard, 28, Juan Mata,32, Diogo Dalot 21 na Phil Jones, 29, kuongezea bajeti yake ya £80m msimu wa joto. 

Hayo yakijiri Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc, amesema klabu hiyo imepatia kipaumbele kushinda Ligi ya Mabingwa kupitia Bundesliga wanapojitahidi kusalia na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kwa “muda mrefu iwezekanavyo”. 

by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE