Wahudumu wa boda boda katika kituo cha kibiashara cha Malekha eneo bunge la Malava kauti ya Kakamega wametamaushwa na kisa ambapo mmoja wa wakaazi eneo hilo alikibomoa kibanda walichokuwa wamejengewa eneo hilo kwa kusudi la kuwasaidia kuendesha biashara yao kwa madai kuwa kimejengwa shambani mwake.

Wakiongozwa naye Jomo Okanga ambaye ni mwenyekiti wao, wahudumu hao wameelaani vikali kitendo hicho wakihoji kuwa hiyo ni njia moja wapo ya kuathiri miradi ya maendeleo katika soko hilo.

Aidha wamewataka viongozi pamoja na vyombo vya usalama kuingili kati na kutatua swala hilo na vile vile wakimtaka mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ni kisa ambacho kimekashifiwa vikali na mwakilishi wa wadi ya Butali Chegulo Kevin Mahelo ambaye amewataka wananchi kuheshimu mali ya umma.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE