Mfanyabiashara maarufu eneo la Uasin Gishu Bundotich Zedikiah Kiprotich almarufu kama BUZEKI amejiuzulu kama katibu mkuu wa Chama Cha Mashinani (CCM) kinachoongozwa naye aliyekuwa gavana wa Bomet Isaac Ruto.

BUZEKI amesema auamuzi huo umeafikiwa baada ya Isaac Ruto kujiunga na naibu rais William Ruto katika kile kinaonekana ni njia mojawapo ya kujijenga kisiasa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Ikumbukwe kwamba, BUZEKI alikuwa miongoni mwa wagombea wa ugavana Kaunti ya Uasin Gishu katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 ila akashindwa na gavana wa sasa Jackson Mandago ambaye anaendeleza utawala wake kwa awamu ya pili.

Story By Alovi Joseph

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE