Maafisa wa polisi eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega  wanamsaka mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumnajisi msichana mmoja wa miaka 25 katika kituo cha biashara cha Harambee

Kulingana na mwathiriwa ambaye jina lake tumelibana anasema aliabiri gari kutoka mjini Kakamega akielezea nyumbani kwa dadake maeneo ya Khabukoshe  eneo bunge la Matungu na alipofika katika kituo cha biashara cha Harambee nyakati za jioni alishuka  na alipokuwa akiwasiliana na dadake kwa simu ili amchukuwe  karibu na shule ya msingi ya Bulimbo , mshukiwa huyo alimkaba koo  na kumnajisi .

Anasema kuwa baada ya kisa hicho kutokea, mhudumu wa bodaboda mmoja ambaye alikuwa ametumwa  kumchukuwa aliwasili na kumpata na mshukiwa huyo ambaye alimtambua na wakaripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Harambee ambapo walimkamata muhusika japo  aliponyoka kutoka mikononi mwa maafisa wa polisi baada ya kumuuma afisa mmoja  mdomo wake.

Ni kisa ambacho kilikashfiwa na wenyeji wa eneo hilo wakiongozwa na dadake mwasiriwa kwa jina Lawiya Washika ambaye ameitaka idara ya polisi kumkamata mshukiwa na kumchukulia hatua kali za kisheria .

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE