Maafisa wa polisi mjini Kakamega wanamsaka mwanaume kwa jina Ben Khatondi mwenye umri wa miaka 21 kutoka Muraka eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega anayedaiwa kumficha mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 nyumbani kwake kwa zaidi ya majuma mawili kabla ya kumfukuza huku akisalia kwa njia panda mjini Kakamega akihofia kurejea nyumbani kwao Kaimosi kaunti ya Vihiga.
Kulingana na Carolyne Ambalo si jina lake halisi anasema alijipata kwenye mtego wa mwanaume huyo baada ya kuukalia mtihani wake wa darasa la nane mwaka wa 2019 katika shule ya msingi ya Buhunyilu na baada ya karo ya kujiunga na shule ya upili kushindikana ndipo alisafiri hadi Muraka kwa mjomba wake ambako amekuwa akiishi; kabla ya kukutana na Ben Khatondi ambaye ni mshukiwa na kumlaghai awe mpenziwe kuwa angelimsaidia kurejea shuleni.
Baada ya kuishi naye kwake kwa majuma mawili mapema leo akamtoa nyumbani huku akimweleza alikuwa anasafiri Kisumu na hivyo basi angelimuhitaji baada ya kurejea.
Ni kisa ambacho kimekashifiwa vikali na wakaazi wa mji wa Kakamega wakiongozwa na Maleb Khatioli huku wakiwataka wazazi kuajibikia wanao haswa msimu huu wa janga la covid 19 ambapo nyingi ya familia zimetelekeza wanao na kuwataka maafisa wa polisi kuharakisha na kumtia mbaroni mshukiwa huku wazazi wa msichana huyo john milimu na jackiline milimu wakihitajika kufika kituo cha polisi cha Kakamega ya kati kumchukuwa mwanao.
Kaunti ya Kakamega kwa kipindi cha miezi sita imerekodi idadi ya juu ya visa vya kudhulumia kwa watoto ikipata hadi asilimia 37 huku wingi wa visa hivyo vikitekelezwa na watu wa karibu sana wa wasiriwa
By Lindah Adhiambo