Ili kukwamua wenyeji wa Nambale hasa vijana mwanaharakati wa kisiasa nchini Antony Buluma Samba ameelezea kuwepo na umuhimu wa wenyeji wa eneo bunge hilo kuchagua vijana ambao wana uwezo wa kutangamana na viongozi wengine nchini na kuleta raslimali ambazi zitasaidia kupunguza kiwango cha umaskini na ukosefu wa ajira.

Akiongea katika eneo la Mungatsi kaunti ndogo ya Nambale wakati wa mkutano na wazee kutoka eneo bunge hilo Buluma ameelezea kusikitisha jinsi wenyeji wa Nambale wamesalia nyuma kutokana na uongozi mbaya na sasa hali hiyo inaweza tu kubadilishwa kwa kuchagua vijana wenye maono.

Aidha Buluma ambaye pia ni mkurugenzi wa muungano wa vijana bungeni almaarufu Young Youth Parliamentarians amekosoa viongozi wanachaguliwa eneo bunge hilo kwa kukosa ubunifu na kutegemea pesa za CDF huku vijana wakisalia kuteseka.

Usemi huo umeungwa mkono na baadhi ya akina mama katika eneo hilo wakiongozwa na Dorcas Kadima ambao wamesema kuwa vijana wengi eneo bunge la Nambale wanateseka kwa kukosa viongozi wanaojali maslahi yao na badala yake kujitakia makuu.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE