Hisia kinzani zinashuhudiwa kufuatia agizo la serikali ya kaunti ya Kakamega kuagiza miili kutolewa kwenye hifadhi za maiti na kuzikwa moja Kwa moja huku familia nyingi zikikiuka kwa kudai kuwa ni kinyume na mila za jamii ya waluhya

Mzee Nashon Tindi anaitaka serikali kughairi msimamo na kuruhusu jamii kuandaa mazishi la muhimu ni kuzingatia masharti ya afya

Itabidi serikali ibadilishe msimamo yake sisi hatuwezi kutoa mtu wetu mochari na tumzike hiyo siku hiyo haiwezekani na tunavunja mila na sheria zetu kama wazee. sisi cha muhimu nikuzingatia masharti ya kutoambukizana corona na kila kitu itakua sawa na hatutakosea marehemu heshima zake.


Familia nyingi tayari zinakiuka agizo na kusema masharti hayo yanakosa heshima kwa marehemu.

Mwenyekiti wa mafundi wa maghari mjini Moses Musundi ambaye alimpoteza mamake mzazi  bi Sofia Andanje  eneo la Sichirai wadi ya Sheywe amesema hawangeweza kutii masharti hayo na ikawabidi kuutoa mwili siku moja kabla ya mazishi

Sisi hatungeweza kutii masharti hayo na ndio maana tumetoa mwili jana na tunazika leo. kwahivyo hiyo masharti inamkosea marehemu heshima kabisa na hapo sidhani kama wananchi watafata hao

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE