Afisa wa jeshi katika kitengo cha Kenya Army Warrant Officer 2 Isiah Ambata Likuyani aliyekuwa akihudumu kwenye mkoa wa bonde la ufa amestaafu rasmi kutoka huduma za kijeshi
Kwenye hafla iliyoandaliwa nyumbani kwake Buyokha, kwenye eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega Ambati amesema ni safari iliyogharimu miaka 39 aliyohudumu kwenye kitengo cha usalama huku akimshukuru mwenyezi Mungu kwa kumwezesha kukamilisha vyema safari hiyo na kuwashukuru wote walioshirikiana naye kazini
Ambata amesema upendo alioanao kwa taifa hili pamoja na maombi kutoka kwa familia yalimwezesha kukamilisha kazi hiyo bila vizingiti
Nao wakewe afisa Isiah pia wakimshukuru kwa ueledi wake na kumkaribisha nyumbani baada ya kuhudumu serikalini kwenye wizara ya usalama, wamemtaja kama baba anayejali matakwa ya familia yake bila mapendeleo
Sifa hizo zikienezwa na wanawe pia wakisifia ujasiri wake pamoja na upendo alionao kwa familia yake na kumkaribisha nyumbani baada ya kustaafu
By Sajida Javan