Serikali ya kaunti ya Kakamega imetangaza kuwafuta kazi wahudumu wake wa afya wanaoshiriki mgomo na kuajiri wahudumu wengine wapya kuanzia juma lijalo.
Akizungumza katika eneo bunge la malava gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Oparanya amewasuta wahudumu wa afya kwenye kaunti hiyo kwa kuendeleza mgomo huo bila kuzingatia sekta zingine muhimu.
Oparanya ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magava nchini ameinyoshea kidole cha lawama serikali ya kitaifa kwa kuchelewesha fedha za kutekeleza maendeleo mashinani akitaja hatua hiyo kama ya kuyumbisha ugatuzi kote nchini.
Wakati uo huo gavana Oparanya amewahimiza wananchi kuendelea kufuata masharti ya serikali kupitia kwa wizara ya afya katika kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona.