Gavava wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Ambesa Oparanya pamoja na Naibu Gavana Phillip Kutuma na Mwakilishi wadi wa Sango Kennedy Kilwake hii leo wamezuru eneobunge la Likuyani kwa minajili ya uziduzi wa baadhi ya miundo misingi eneo hilo
Hafla hiyo ambayo imefanyika katika ofisi za kaunti wadi ya Sango Oparanya amezindua barabara ya kutoka Sango kuelekea Kongoni ambayo inawekwa Lami ili kuimarisha usafiri eneo hilo
Kando na hayo Oparanya amegusia swala la ukulima ambapo wakaazi wa Likuyani wanatarajia kupata mbolea kwa bei nafuu ili kuimarisha sekta ya kilimo
Kuhusu swala la mgomo wa madaktari gavana Oparanya amesema kuwa Mikakati kabambe imewekwa kuhakikisha kwamba wanamaliza mgomo huo.
Story by Samson Nyongesa