Gavana wa kaunti ya Vihiga dkt. Wilbur Otichillo amesema kaunti yake imenunua mtambo wa kutoa hewa ya oxjeni kama njia moja ya kukabili janga la korona.
Akiongea na wanahabari afisini mwake otichillo amesema kaunti yake imenunua mtambo huo kutoa kwa shilingi milioni 62 walizopokea kutoka kwa serikali kuu.
Otichillo ameelezea kusikitishwakwake na hatua ya serikali yake kukosa mgao wa pesa zaserikali tangia mwezi januari mwaka huu jambo analosema limelemaza miradi ya maendeleo.
Aidha amepiga marufuku hulka ya wananchi kula vyakula kwenye hafla za matanga, huku akipongeza wauguzi wa kaunti hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kupokea chanjo ya korona.
By Javan Sajida