Spika wa bunge la Kaunti ya Bungoma Emmanuel Situma amemtaka Gavana Kaunti hiyo Wycliffe Wangamati kufuata sheria katika uagizaji wa fedha kutoka kwa serikali ya Kitaifa na kuwalipa wafanyakazi wa Kaunti hiyo.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, Spika huyo amesema licha ya serikali ya Kaunti ya Bungoma kuagiza pesa za mishahara mwezi Mei, hadi sasa wafanyakazi katika serikali ya Kaunti hawajalipwa.

Aidha Spika huyo amemkosoa Gavana Wangamati kwa kupunguza mgao wa fedha katika bunge la Kaunti hiyo kinyume cha sheria, hali ambayo imeathiri wanakandarasi kutowasilisha baadhi ya bidhaa muhimu huku walinzi katika bunge hilo wakianza mgomo kwa kukosa malipo ya miezi mitatu.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE