TIMU za Ajax, AS Roma na Villarreal ni miongoni mwa vikosi vilivyojiweka pazuri zaidi kufuzu kwa robo-fainali za Europa League msimu huu wa 2020-21 baada ya kubwaga wapinzani wao kwenye mechi za mkondo wa kwanza mnamo Alhamisi usiku.

Roma ambao ni miamba wa zamani wa soka ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) waliwakung’uta Shakhtar Donetsk ya Ukraine 3-0 katika uwanja wao wa nyumbani huku Ajax ya Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) pia wakiwapokeza Young Boys kutoka Uswisi kichapo cha 3-0 jijini Amsterdam, Uholanzi.

Villarreal ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) kwa alama 37, waliwakomoa Dynamo Kyiv ya Ukraine 2-0 huku Granada wanaokamata nafasi ya 10 kwenye jedwali la La Liga wakisajili matokeo sawa na hayo dhidi ya Molde ya Norway nchini Uhispania.

Hayo yakijiri Chelsea huenda ikamuuza mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner mwisho wa msimu huu mwaka mmoja baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka RB Leipzig kwa dau la £54m.

by Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE