Kwa mara nyingine gavana wa kaunti ya Kakamega ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la gavana nchini Wycliffe Ambetsa Oparanya ameshikilia kauli yake ya kupiga kalamu wahudumu wa afya ambao bado wanagoma kufikia wiki lijalo akifichua kuwa tayari mchakato wa kuawaajiri wauguzi 60 kwa awamu ya kwanza umekamilika
Akihutubu mjini Kakamega baada ya kufungua rasmi kikao cha mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa baraza la utawala kwa jamii, gavana Oparanya amesisitiza kwamba hatatishwa na yeyote kwa uamzi ambao tayari ameufanya wa kuwapiga kalamu wahudumu hao akidokeza kuwa matakwa ya wahudumu wa afya waitisha kwa sasa si ya serikali za kaunti
Gavana huyo anashangaa ni kwa nini wahudumu hao wa afya hawarejei kazini na ilhali kama kaunti wametekeza wajibu wao wa kuwapa bima, na nyongeza ya mishahara walipogoma mara ya kwanza
Story by Richard Milimu