Mbunge wa Matungu Peter Oscar Nabulindo amesikitikia huduma duni katika hospitali ya Matungu ikiwemo ukosefu wa dawa ,wagonjwa wa kiume na wa kike kulazwa kwenye wadi moja kati ya changamoto zingine nyingi huku akitaka serikali ya kaunti ya Kakamega kuingilia kati kuona kuwa hospitali hiyo inawahudumia wagonjwa ipaswavyo.

Mbunge huyo, aliyezuru hospitali hiyo baada ya wahudumu wa afya pamoja na wagonjwa kulalamika, amesikitikia hali duni ya mazingira kwenye hospitali hiyo ikiwemo ukosefu wa vifaa na dawa , upungufu wa wahudumu wa afya, hali mbovu ya miundo msingi, wagonjwa kubeba chakula kutoka nyumbani na wagonjwa wa kike kulala katika wadi moja na wa kiume 

Nabulindo ameisuta serikali ya kaunti ya Kakamega kwa kukosa kuajibikia idara ya afya ambayo iko chini ya serikali za kaunti

Mbunge huyo ameitaka serikali hii kuajibika huku akitoa wito kwa serikali kuu kupitia wizara ya afya kuingilia kati la sivyo hospitali hiyo ifungwe. 

Kwa upande wake waziri wa afya katika kaunti ya Kakamega DK. Collins Matemba ameinyosheeya kidole serikali kuu kwa kutotuma fedha inavyostahili huku akisema kuwa huduma nyingi zimeathiriwa kutokana na ukosefu wa pesa za kuzifadhili

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE