Uchumi wa kenya umezoroteka sana mwaka huu kutokana na janga la corona ikilinganishwa na miaka za apo awali. Ni usemi wake mchungaji ibrahim gitau shiyonga wa kanisa la full gospel churches of kenya mjini kakamega.
ajizungumza na idhaa hii mjini kakamega huyu anasikitishwa na jinsi wananchi wa mashinani wanavyo kosa fedha za kuwatosha kujimudu kwa mapato yao ya kila siku kama vile chakula
Kwa sasa hivi wanannchi wa mashinani hawapati fedha za kuwatosha maanake hata chakula hawana. Pesa wanazo pata hutumika ile wakati tu wanapata
anasema kuwa ukosefu wa fedha umetokana na wananchi kupoteza kazi, biashara kadhaa kufungwa hasa biashara ndogondogo na hivyo kufanya mahitaji kuwa mengi katika jamii ya watu wa mashinani na zile ambazo hazijiwezi.
Kuna ukosefu mkubwa wa fedha na mahitaji yamekua ni mengi. Watu wengi wamepoteza kazi, biashara kadhaazimefungwa haswa wale waliokuwa wakifanya biashara ndogondogo.
hata hivyo anawaomba wakuu washule kuwavumilia wazazi wakati shule zinapofunguliwa hivi karibuni wakizingatia kuwa uchumi umezorota nnchini na kuwaruhusu wanafunzi kusoma bila mahangaiko.
Sasa hivi shule ziko karibu kufunguka na mabo hayako sawa na wakati wa\nafunzi watakua shule tunaomaba waalimu wakuu wa shule kuvumilia wazazi maanake uchumi hauko sawa.
By Imelda Lihavi