Hali ya maisha kupanda na kuongezeka kwa visa vya utovu wa nidhamu ni miongoni mwa vilio vya wazazi wakati shule zinapotarajiwa kufungwa wiki hii.
Shule zinatarajiwa kufungwa kwa ajili ya likizo na pia kuwapa wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nne nafasi ya kukalia mitihani yao ya kitaifa.
Wazazi wanalalamikia muda mrefu wa likizo waliopewa wanafunzi kukaa nyumbani.
Wakiongozwa na mkaazi wa Kakamega mzazi Juma David,
“wazazi hatuna chochote sai bei ya chakula ilipanda watoto wanakuja nyumabani na sasa hatuwezi kaa nyumbani na watoto tukiwaangalia lazima tutokea tutafute. Hii likizo ni ndefu sana wangepewa ata likizo ya mwezi moja ama ata wiki tatu ingekua afadhali ndo tujue tu tunatafuta school fees sio chakula mara school fee mara watoto wenyewe wakibaki nyumbani hatuna hiyo mda ya kuwaangalia na pia hatuna pesa ya kuandika wafanyikazi wa nyumba na ata tukiwaandika hatujui kama watoto wenyewe watakua salama.” alisoma Juma
by Lavin Watsetse