Huku ikisalia masaa machache tu kwenye uchaguzi mdogo wa kumchagua mbunge wa eneola Matungu,,tetezi kadhaa zinazidi kuibuka miongoni mwa viongozi kutoka mirengo mbalimbali ya kisiasa ikiwemo ule wa UDA na ANC

Akizungumza na wanahabari mwaniaji wa kiti hicho kwenye chama cha UDA Alex Lanya, mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali na Paul Posho wanazidi kutoa wito kwa tume ya IEBC kumrekebisha afisa msimamizi wa kuhesabu kura hizo kwani anadaiwa kuwa mfanyikazi wa kaunti ya kakamega na wanahofia kuwepo kwenye wizi wa kura hizo

Ni kauli iliyoungwa mkono na kinara wa chama cha anc msalia mdavadi na viongozi kutoka chama hicho

Viongozi hao aidha wamesema kuwa kuna gari aina ya ambulence ambayo inatembea katika maeneo ya matungu na kuna madai kuwa imebeba silaha butu na kuhofia kutokuwepo  kwa usalama kwenye uchaguzi huo huku wakitka maafisa wa usalama kuangazia madai hayo

Pia wametaka wakaazi wa eneo hilo kuwa waangalifu na barakoa watakaopatiwa na mtu yeyote kwani kuna madai kuwa barakoa spesheli zinapeanwa kwa wakaazi wa matungu na huenda zikaleta madhara miongoni mwao

Viongozi hao wametaka maafisa wa polisi kusimamisha mikutano ya hadhara inayozidi kufanywa kwenye mikahawa kwani siku za kampeni na mikutano zilikamilika

Kamishina wa tume ya IEBC Abdi Guley amedhibitisha kuwa afisa huyo kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kakamega ameondolewa kusimamia kura hizo

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE