Kituo hiki kimezidi kupongezwa kwa kuibuka kama kituo nambari moja nchini kwa vipindi vya watoto kwenye mashindano yaliyokamilika ya kuza awards mwaka 2021
Wa hivi punde kutoa pongezi yake ni mwaniaji wa kiti cha ubunge kwenye eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega Samuel Wekesa Wekulo ambaye amepongeza bodi ya wasimamizi wa kituo hiki,wanahabari na pia mashabiki wote kwa ushindi huo muhimu kwenye mashindano hayo
Wakati uo huo Wekesa amewataka viongozi nchini kuheshimu uamuzi wa koti siku zote bila kujali ni kesi na uamuzi upi umetolewa na majaji
Kauli yake ikiwalenga viongozi ambao hawajakubaliana na uamuzi wa majaji 5 kwenye mahakama ya juu wa kusitisha mpango wa kubadilisha katika kupitia mfumo wa BBI
Wekulo amewataka kukata rufaa iwapo hawajaridhishwa na uamuzi huo na kuwataka viongozi kuwa wenye unyenyekevu
By Javan Sajida