Wataalamu wa maswala ya kisheria na kikatiba wanatilia shaka msukumo wa rais kwenye swala zima la katiba
Mwanasheria kutoka kaunti ndogo ya Navakholo wakili Edwin Wafula amesema kuwa huwenda rais ana nia fiche kwenye mchakato mzima wa BBI
Wafula aidha amepinga uwezo wa kamati ya BBI kuunda maeneo zaidi ya bunge nchini
Wakili huyo kwenye mahakama kuu ya Kakamega amepuuzilia mbali uwezekano wa kura ya maoni kutekeleza kabla ya uchaguzi mkuu
Vilevile ameonya kuwa taifa hili huwenda likatumbukia kwenye mgogoro wa kikatiba iwapo rais atazidi kupuuza maagizo ya mahakama
By James Nadwa