Watu 335 zaidi waambukizwa ugonjwa wa COVID-19 na kufikisha idadi ya walio ambukizwa kuwa jumla ya 97,733. visa hivyo  vipya vimetokana na sampuli 5,424 zilizopimwa chini ya saa ishirirni na nne

Kulingana na taarifa ya Alhamisi wakenya walioambukizwa ni 307 na raia wa kigeni wakiwa 28, wanaume 233 na wanawake 102. visa hinyo ni kati ya umri wa mwaka mmoja na umri wa miaka 94.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 102, ikifuatwa na Meru kwa visa 46, Makueni 40, Nyeri 19, Kajiado 14, Embu 13, Mombasa 12, Kiambu 11, Nakuru 9, Nyandarua 9, Busia 9, Samburu 8, Kirinyaga 6, Machakos 5, Kitui 4, Turkana 4, Laikipia 3, Uasin Gishu 3, Siaya 3, Kilifi 2, Marsabit 1, Narok 1, Muranga 1 na Taita Taveta 1.

Wagonjwa 340 wamethibitishwa kupona, 216 kati yao walikuwa kwenye mpango wa kutibiwa nyumbani ilhali 79 walikuwa katika hospitali mbalimbali. idadi hiyo inajumuisha waliopona kutokana na COVID-19 kufikia sasa ni 80,306.

Wagonjwa wanane wamefariki katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya waliofariki hadi 1,702.

story by Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE