Huku zikiwa zimesalia siku mbili kuelekea katika uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha Matungu utakaoandaliwa mnamo Machi nne viongozi kutoka mirengo tofautitofauti wameendeleza kampeni maeneo tofautitofauti ya Matungu.
Akizunguza katika maeneo ya Mayoni katika kampeni za kumpigia debe Oscar Peter Nabulindo muaniaji wa kiti cha ubunge katika tiketi ya chama cha ANC Musalia amemsuta kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwa mbinafsi baada ya ndugu ya Oburu Odinga kusema Raila ndiye atakaye ipeperusha bendera ya chama cha ODM katika kinyang’anyiro cha uraisi mwaka 2022.
Aidha Musalia Mudavadi akiwa ameandamana na viongozi wengine kumpigia debe Oscar Nabulindo wamewasuta wapinzani wao kwa kuwatishia wapiga kura na hata kuchukuwa vitambulisho vya kupigia kura huku seneta Cleophas Malala akimtahadharisha katibu wa ODM Edwin Sifuna kwa njama ya kuleta vurugu siku ya kupiga kura.
Mrengo wa ODM ukiongozwa na katibu Edwin Sifuna,Raphaili Wanjala,Kizito Mkali nao umeendeleza kampeni za kumpigia debe David Were huku Oscar Sudi,Bonny Khalwale,Benjamin Washali ,Aisha Juma wakimpigia debe Alex Lanya wa UDA.
Kwa mjibu wa John Kirui afisa wa IEBC ambaye amesimamia zoezi hilo amesema wao kama tume ya uhuru na mipaka wamejipanga na kuwa kura itakuwa ya huru na haki.