Kocha wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anapanga kumsajili kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, wa miaka 33, ambaye pia alikuwa chini yake katika klabu ya Manchester United. Fellaini kwa sasa yupo na klabu ya Shandong Luneng ya Uchina toka Februari 2019 alipoihama United.

Huku Klabu ya Leicester City ipo mbele ya Manchester United na katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille Boubakary Soumare mwenye umri wa miaka 22. 

Hayo yakijiri Manchester United wanamtaka ‘kwa udi na uvumba’ beki wa klabu ya Villarreal na Uhispania Pau Torres mwenye umri wa miaka 24, ambaye pia anawaniwa na vigogo wengine wa soka barani Ulaya klabu za Bayern Munich na Real Madrid. 

Kando na hayo Manchester united ,Arsenal ,Roma pamoja na Villariale walijikatia tiketi ya ya kufuzu Nusu fainali katika ligi kuu Bara Europa hapo jana 

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE