Kanisa katoliki limepiga marufuku wanasiasa wote nchini kuhutubia watu kanisani wakati wa ibada.

Mwenyekiti wa baraza la waumini, askofu mkuu Antony Muheria amewaagiza wanasiasa kuenda kanisani kuhudhuria ibada tu kisha kuondoka kama waumini wengine.

Askofu Muheria amewaomba wanasiasa kupatia kanisa heshima na kuwaeleza  kwamba watachukuliwa tu kama waumini wengine pale kanisani.

Kanisa katoliki limesema kuwa halitaruhusu wanasiasa kuzungumza katika kanisa zetu. Wanasiasa ikiwa mnakuja kuabudu katika kanisa zetu, mnakaribishwa lakini kaeni kama waumini wengine na tafadhali musitarajie kuhutubia watu. NJooni Muabudu kasha muende. Askofu alinena

Askofu huyo amesema kwamba inasikitisha  kuona kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanalazimisha kupewa nafasi ya kuhutubia waumini kila wanapoenda kanisani.

Askofu muheria amewaomba  wanasiasa hao kuzungumza na mungu wala sio waumini kila wanapoenda kuabudu kanisani.

Mungu anakujua wewe na anajua kile unahitaji. Nenda kwake usije kwetu, usitake tukusifu, tafuta Baraka za Mungu kivyako kama mtu mwingine yeyete. Acha tupatie nyumba ya Mungu na mahali patakatifu heshima. Patwa na aibu wakati unapo simama pale kuzungumza siasa na matusi kwani unaalikalaanamaishanimwako. Huu ni ujumbe kwa wanasiasa wote

Askofu amewaomba maaskofu wengine na mapadri kuwa imara katika utekelezaji wa agizo la kutowaruhusu wanasiasa kuzungumza kanisani.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE