Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega daktari Boni Khalwale ameisuta serikali ya kaunti hiyo chini ya uongozi wake gavana Wycliffe Oparanya kwa kukosa kuweka mikakati kabambe ya kuwasaidia wachimba migodi katika kaunti hiyo jambo ambalo limechangia wengi wao kuangamia kwenye timbo ambazo ziko eneo hilo
Akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Bushsngala eneo bunge la Ikolomani baada ya kuzuru eneo la mkasa ambapo watu watano waliangamia Kwa mgodi na wengine kujeruliwa, khalwale amemsuta gavana oparanya kwa kufumbia jicho masaibu ambayo yanawakumba wachimba migodi wadogo wadogo
Khalwale vile vile amemkashifu rais Uhuru Kenyatta kwa kukosa kutoa utaratibu kwa wizari ya madini na mafuta ya humu nchini kumtafuta mwekezaji ambaye angeekeza eneo hili baada ya kugunduliwa kuwepo kwa dhahabu jinsi ilivyo fanyika na mafuta kaunti ya Turkana
Aidha Khalwale amewataka wabunge ambao hutoka maeneo ambayo huchimbwa dhahabu kuhakikisha kwamba matakwa ya wananchi hao inawakilishwa ipasavyo wakiwa bungeni
By Richard Milimu