Katibu mku wizara ya afya katika kaunti ya Busia amesema kuwa tangu kutatuliwa kwa sekta hiyo muhimu kaunti ya Busia imepiga hatua haswaa katika kuyaboresha mazingira wanayohudumiwa wagonjwa kwenye hospitali kuu ya Busia na nyingi ya zahanati katika kaunti hiyo.
Kwenye taarifa kwa wanahabari dkt Omeri amesema kuwa licha ya changamoto za hapa na pale,kama wizara imejizatiti kuhakikisha kuwa angalau hospitali na zahanati zinatoa huduma bora kwa wakaazi,
Kuhusiana na jinsi wizara inakabiliana na covid-19 katibu huyo amesema kuwa kaunti ya Busia imejipanga na vitanda vya dharura ila amesema kuwa kama kaunti zingine tu wana changa moto za mashine ya Oxygen,
Dkt Omeri aidha ameitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Busia kuchukua taadhari na kuyafuata masharti ya serikali ili kupiga cheki juhudi za serikali za kuudhibiti msambao zaidi wa virusi vya covid -19 .
Ikumbukwe kuwa taakrimu za serikali kuu zinaonyesha kuwa kaunti ya Busia ni miongoni mwa kaunti zilizo kwenye hatari ya msambao wa covid ikizingatiwa kuwa ipo mpakani mwa kenya na uganda,
By Hillary Karungani