Naibu gavana wa kaunti ya Busia Moses Mulomi amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo imepokea dosi 7000 za chanjo aina ya modena ili kukabili msambao wa virusi vya covid 19
Mulomi amesema kuwa hii itawezesha kaunti hiyo kudhibiti ugonjwa huo akiwataka wakaazi kujitokeza na kupokea chanjo hiyo
Naibu huyo wa gavana amedokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo imejitolea kuboresha viwango vya afya ikiwemo kuhimarisha huduma za matibabu kwenye hospitali za kaunti hiyo
By James Nadwa