Muungano wa kiuchumi Kaskazini mwa Bonde la Ufa (NOREB) wameweza kuungana na kaunti zingine  ishirini na kutenga fedha za wakulima ambazo zitawasaidia kuwachanja mifugo dhidi ya maradhi ya miguu na midomo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji  wa Muungano wa kiuchumi Kaskazini mwa Bonde la Ufa (NOREB )Dominic Biwott alisema haya akizungumza na waandishi Wa habari na kusema kuwa uuzaji wa mifugo kutoka eneo hili limeathirika pa kubwa na maradhi ambayo yamekuwa yakiangamiza mifugo.

Hata hivyo Biwott ameongeza kuwa ajenda ya mkutano uliokuwa hivi leo wameangazia maswala ya wanawake walivyoathirika hasa wakati wa janga la korona wataweza kuweka miradi ambayo itawasaidia kumudu kimaisha, bali na hayo vijana watatumika kuhimiza amani hasa wakati wa siasa.

Story by Sharon Lukorito

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE