Mamlaka ya kutathmini ubora wa vyeti nchini (Kenya National Qualificationa Authority) imenzisha mpango wa kupiga marufuku vyeti vyote ambavyo havijaidhinishwa.

Kwenye taarifa kwa wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dakt.Juma Mukhwana amesema kuwa tayari wamezindua wavuti utakaotoa nafasi kwa wakenya ili kuripoti vyeti bandia

Katika njia hii mpya mtu yoyote anaweza tumia wavuti wa rev@knqa.go.ke/cheti-mwitu na kuwasilisha taarifa itakayosaidia kupata na kuripoti cheti bandia.

“Today we have longed online platforms where Kenyans can report fake certificates. This to ensure that as the authority we are eradicating fake certificates in Kenya. “

Wakati uo huo Mukhwana amesema wanalenga kufanya uhamasisho katika taasisi mbalimbali ili kuepusha visa ambapo watu wenye vyeti bandia wamepewa nafasi za ajira kinyume cha sheria.

  Story by Sajida Javan

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE